Baba mzazi wa Lulu nae alikuwepo mahakamani hapo.
Mwigizaji
Maarufu wa filamu za Kibongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo majira ya saa
nne asubuhi amepandishwa kizimbani kwa mara ya pili katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa shitaka la kumuua
Steven Kanumba. Baada ya kusomewa shitaka hilo na Mwendesha Mashitaka
Mkuu wa Mahakama hiyo Elizabeth Kaganda mbele ya Hakimu Rita Tarimo
hakutakiwa kujibu lolote. Mwendesha Mashitaka huyo alisema upelelezi wa
kesi hiyo bado haujakamailika hivyo kesi hiyo iliahirishwa mpaka Mei 7
mwaka huu.
PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS/GPL
No comments:
Post a Comment